Haji Manara Kufukuzwa Na Gsm!
Baada ya sakata Linaloendelea mitandaoni kumuhusu Manara ambapo anatajwa kuongea maneno tata, baada ya (voice note) kuvuja - baadhi ya voice notes (sauti fupi) zikimuongelea #Alikiba kuwa hajui kuimba ni mbana pua, ikaenda mbali zaidi voice notes hizo (sauti fupi) zikimuongelea vibaya mke wa Boss “GSM” kuwa anafanya surgery, uturuki, na mambo mengi zaidi…
‘Mwijaku hapo jana kupitia ukurasa wake wa instagram ameweka wazi kuwa “Kesho inshaallah pale salamander tower Mzungu atakutana na Notes yake tayari “WANAMFUKUZA” Asante management kwa kutambua heshima ya madam sasa tuone na hio online yake mtakuwa mnashinda wapi”- Mwijaku. Ikiwa na maana kwamba leo sasa- Huenda Manara akapoteza ujira wake kuwa Balozi wa Gsm companies.
Ikumbukwe GSM ndie mfadhili mkuu na mdhamini wa klabu hiyo. GSM amekuwa na mchango mkubwa katika maendeleo ya Yanga, akitoa msaada wa kifedha na vifaa mbalimbali kwa timu. Kwa mfano, mnamo mwaka 2022, Yanga iliingia mkataba wa udhamini na GSM wenye thamani ya Shilingi bilioni 10.9, hatua iliyosaidia kuimarisha uwezo wa kifedha wa klabu hiyo .
Je #HajiManara atasamehewa?